Monday, August 03, 2015

ZIARA YA NHC DODOMA FAMILY DAY KWENDA MIKUMI NATIONAL PARK


Mwanzo wa safari yetu kutoka Dodoma ofisini kuelekea Mikumi National Park Morogoro. Picha zote za Shirika la Nyumba la Taifa.

 Wafanyakazi na familia zao wa mkoa wa Dodoma tumeshaingia Mkoa wa Morogoro tayari kwa kuanza  safari ya kuelekea Mikumi Nationa Park.
 Hapa ndio tunaingia kwenye viunga vya Mikumi Ntional Park.
 Wafanyakazi na familia zao wakiwa mbele ya lango la kuingia mbugani

 Twiga wakiwa mbugani, Mnyama anaetumia miguu yake kupambana na adui, ni vigumu kuuliwa na simba kwasababu ya shingo yake ndefu.
 Swala wakiwa mbugani, dume huwa na pembe na  inasemekana dume mmoja anamiliki majike 40

 Nyumbu wakiwa Mbugani, ni wanyama wanao zaliana sana, na ndio chakula hasa cha simba.
Tembo wakiwa Mbugani, Hutumia pembe zake kujihami na adui na hutembea kwa makundi kulingana na rika na uwezo wa kupambana na adui.
 Wafanyakazi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye gari mbugani wakichungulia nje baada ya kumwona Tembo.
 Simba jike  akiwa amejipumzisha chini ya mti
 Meneja wa Mkoa wa Dodoma ndugu Itandula Gambalagi akitoka kuangalia mamba na kiboko bwawani .
 Hapa ndio sehemu lilipo bwawa lenye mamba, viboko na ndege wa majini.

  
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba mkoa wa Dodoma wakibadilishana mawazo na watalii wengine ndani ya mbuga ya wanyama Mikumi

No comments: