Wednesday, August 05, 2015

RAIS KIKWETE KUZINDUA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Thomas Samkyi, (pichani kati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Benki hiyo,Kinondoni kuhusu uzinduzi wa benki hiyo utakaofanyika Agosti 8, 2015,jijini Dar. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki, Bi Rosebud Violet Kurwijila.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bi Rosebud Violet Kurwijila akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),katika ofisi za Benki hiyo jijini Dar mapema leo kuhusu uzinduzi wa benki hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Thomas Samkyi, na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema asubuhi ya leo

 Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua rasmi benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, ambayo inalenga kuanzisha mtizamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali, kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo. Benki hiyo inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa sekta ya kilimo ambayo imeajiri zaidi ya aslimia 70 ya Watanzania.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa ngazi mbili: ngazi ya kwanza itahusisha uzinduzi wa Makao Makuu ya TADB jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 7 ya mwezi huu; ambapo ngazi ya pili itahusisha uzinduzi rasmi wa TADB mbele ya wadau wake wakuu ambao ni Wakulima, kwenye Maonesho ya Nane Nane Mkoani Lindi, katika kilele cha Siku Kuu ya Wakulima hapo tarehe 8 Agosti 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo yaliyoko Barabara ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa benki, Bwana Thomas Samkyi, alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa benki hiyo ni kuboresha tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali ili kuwezesha uendelezaji wa miundombinu ya kilimo kama miradi ya umwagiliaji, usafirishaji, uhifadhi, mindombinu ya masoko, n.k. ambayo inachangia maendeleo ya sekta ya kilimo.

‘Uanzishwaji wa benki hii unalenga kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo ambayo inaachwa na benki za biashara, ili kuchochea kukua kwa sekta ya kilimo, kwa kutoa mikopo na huduma nyingizezo za uwezeshaji wa kilimo kwa wakulima, ambao wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za kibenki’ alisema Bw. Samkyi.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA PANGANI, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI TANGA

PANGANI, TANGA – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 26, 2025, amezungumza na wananc...