
(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
……………………………………………….
Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.

No comments:
Post a Comment