Monday, August 17, 2015

CCM YATANGAZA UTEUZI WA WAGOMBEA WA MAJIMBO 11 YALIYOKUWA YAMEBAKIA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo mchana,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa wa wagombea Ubunge wa majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa leo Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imefanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia.

Wagombea Ubunge walioteuliwa na majimbo yao kwenye mabano ni:-


1.Ndugu Jerry Slaa                                  -        (Ukonga) Dar es Salaam
2.    Ndugu Edward Mwalongo                      -        (Njombe Kusini) Njombe
3.    Ndugu Venance Mwamoto                     -        (Kilolo) Iringa
4.    Ndugu Raphael Chegeni                        -        (Busega) Simiyu
5.    Ndugu Edwin Ngonyani                         -        (Namtumbo) Ruvuma
6.    Ndugu Mohamed Mchengerwa               -        (Rufiji) Pwani
7.    Ndugu Norman Sigara                           -        (Makete) Njombe
8.    Ndugu Martin Msuha                             -        (Mbinga Vijijini) Ruvuma
9.    Ndugu Joel Makanyanga Mwaka             -        (Chilonwa) Dodoma

Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/08/2015

Post a Comment