Dar Es Salaam
……………………..
BODI ya Usajili wa Wakandarasi (ERB) imetengeneza ajira 1600 iliyotokana na usajili wa makampuni ya ushauri wa kihandisi 160 katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015.
Hayo yamesemwa juzi(Jumanne Agosti 4, 2015) na Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Steven Mlote wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Bodi hiyo katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
Mhandisi Mlote alisema idadi ya wakandarasi waliosajiliwa na na Bodi hiyo imeongezeka katika kipindi hicho kutoka wakandarasi 6868 mwaka 2005 hadi wakandarasi 15,364 mwaka 2015, ikiwa ni ongezeko la wahandisi 8496.
Aidha Mhandisi Mlote alisema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na ongezeko la wakandarasi wanawake kutoka wakandarasi 20 waliosajiliwa mwaka 2011/12 hadi kufikia wakandarasi 80 katika kipindi cha mwaka 2013/14 na hivyo kufanya wakandarasi wataalamu wanawake kufikia 176 hadi sasa.
Akifafanua zaidi Mhandisi Mlote alisema kuwa Bodi imeendelea kutembelea na kukagua hali ya uhandisi katika Halmashauri zote za Tanzania Bara. “Kaguzi hizo zimewezesha halmashauri nyingi kuajiri wahandisi na kuwatumia katika miradi ya ujenzi” alisema Mhandisi Mlote.
Mhandisi Mlote alizitaja changamoto zinazoikabili Bodi hiyo ni pamoja na idadi ndogo ya wanandisi kukidhi mahitaji ya nchi, uwezo mdogo wa kifedha na vitendea kazi na asilimia 69 ya wahandisi wa Halmashauri za Wilaya kuskosa sifa za kuongoza idara za ujenzi.
Bodi ya Usajili wa Wahandisi iliundwa mwaka 1997 chini ya sheria ya Bunge namba 15 ya mwaka 2007, na miongoni mwa majukumu ya bodi hiyo ni kuratibu na kusimamia mienendo na shughuli za kihandisi zinazofanywa na Wahandisi na Makampuni ya ushauri wa kihandisi nchini.
No comments:
Post a Comment