Tuesday, August 18, 2015

BENKI YA EXIM TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 18 YA KUANZISHWA KWAKE.

 Afisa  Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania akizingumza na baadhi ya wafanyakazi  pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo  wakifurahia kwa pamoja wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita
 Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.


Exim Bank imeadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwake huku uongozi wa benki hiyo ukiahidi kuboresha zaidi huduma zake hasa katika kipindi hiki ambacho sekta benki imetawaliwa na ushindani mkubwa.

Benki hiyo iliyoanza kutoa huduma zake mwezi Agosti,1997 ikiwa na tawi moja jijini Dar es Salaam kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini  na matawi saba nje ya nchi huku pia rasilimali yake ikitajwa kuwa na thamani ya sh. trilioni 1.1 hadi kufikia mwezi juni mwaka huu.

Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha baadhi ya waafanyakazi na wateja wa benki hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ukweli kuwa benki hiyo inafanya kazi chini ya bodi ya wakurugenzi iliyo imara.

“Siku kama ya leo miaka 18 iliyopita ndio benki yetu ilianzishwa. Leo benki ya Exim imesaidia ukuaji wa biashara  ndani na nje ya nchi na tunashukuru kuona kwamba baadhi ya wateja wetu wameweza kuhudhuria hafla hii ili tusherehekee pamoja siku hii muhimu,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Selemani mbali ya kuwa na idadi kubwa ya matawi ndani na nje ya nchi pia imefanikiwa kuwa na mashine za kutolea fedha 57 hapa nchini, vituo vya mauzo zaidi 250 na kwa sasa ina matawi kwenye mikoa 16 hapa nchini ambayo yanahudumia takribani wateja 180,000.

“Miaka yote tumekuwa tukiitumia siku hii pia kutathmini ubora wa huduma zetu kwa wateja na ndio maana tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri kila siku. Uhodari wa wafanyakazi wetu imekuwa pia imekuwa ni chachu kwenye mafanikio haya,’’ alibainisha bw. Ponda.

Kwa mujibu wa Bw. Ponda, benki hiyo ndio benki ya kwanza hapa nchini kufungua matawi yake nje nchi ambapo kwa sasa imefungua matawi yake visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.

No comments: