Tuesday, August 18, 2015

ATCL YAREJESHA SAFARI ZAKE KUELEKEA MWANZA.


 Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea Mwanza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya majiji hayo mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
 Abiria wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kuelekea jijini Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati majiji haya mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

 SHIRIKA  la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma  kwa wateja wake hapa nchini.

Safari ya kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.

“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’ alibainisha Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake  mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

Alisema ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.

Akizungumzia na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza mmoja wa abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa kwa huduma hiyo pia alionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa na wahudumu wa shirika hilo.

“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.

Pamoja na kurejesha safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100.

“Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam,’’ aliongeza Fungamtama.

No comments: