Wednesday, August 12, 2015

BENKI YA BARCLAYS YAZINDUA KADI YA ATM DOLA


 Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya ATM ya dola za kimarekani katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather.
   Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akionyesha kadi ya ATM ya Dola za Kimarekani katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather na wamwisho ni 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather, akitoa msisitizo juu ya faida za ATM kadi ya dola za kimarekani kwa wateja watakao zitumia kazi hizo wakati wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali haoa nchini na kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumarakifafanua juu ya matumizi ya ATM kadi za dola za kimarekani katika matumizi ya kawaida katika kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka yanayotumia kadi za ATM hapa nchini, katika mkutano wa uzinduzi kadi ya ATM ya dola, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.
BENKI ya Barclays hapa nchini imezindua kadi ya ATM ya dola hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather wakati akizungumza wakati wa uzinduzi, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.

  alisema “wateja wa Barclays wenye akaunti ya Dola za kimarekani wataweza kutumia kadi hizo mpya wakiwa ndani na nje ya Tanzania kupitia huduma za VISA.”

Kadi hizi mpya zimewekwa kwenye mfumo mpya wa teknohama ambao unawapa wateja usalama zaidi wanapofanya huduma zote za kibenki. Mteja atapata fedha za ndani atakapoitumia kadi hiyo akiwa nchini. Miamala yote ya nje ya nchi itafanyika kwa dola za Kimarekani tu.

Pia amezitaja faida za Kadi za dola kutoka Benki ya Barclays hapa nchini, Inarahisisha malipo ya bidhaa na huduma madukani, hotelini, vituo vya mafuta n.k. nchini na dunia nzima, Utakupo toa hela nje ya nchi kupitia ATM utapata noti za dola za kimarekani,
Inakupa amani ya akili baada ya kukamilisha muamala kwa mtandao na pia inakupa nafasi ya kupata punguzo la bei mtandaoni unapotumia kadi ya matumizi ya Barclays.

Aliendelea kusema “Barclays inawasaidia wateja kunufaika kwa kulenga kuwapatia uzoefu rahisi na kuwasikiliza mahitaji yao.” Barclays inazingatia kila wakati kuwapa wateja wake huduma timilifu za hali ya juu na kwa uzoefu wa hali ya juu.
Post a Comment