Tuesday, May 12, 2015

RED CROSS YAKABIDHI MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO ZANZIBAR


 Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania { RED CROSS } Bwana Shaaban Ali Iddi akikabidhi msaada wa Viatu Pair 90 kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d kwa ajili ya watoto wa familia zilizopata maafa ambao wapo Kambini  Skuli ya mwanakwerekwe “C”.
 Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akiushukuru Uongozi wa Red Cross kwa misaada yao ya Kibinaadamu waliyotoa kwa ajili ya familia zilizopatwa na maafa wiki iliyopita. 
Uongozi wa Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania ukimsikiliza Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d hayupo pichani akitoa nasaha zake baada ya kupokea msaada uliotolewa na Uongozi huo.

No comments:

MMUYA: WANANCHI WANUFAIKE NA UWEKEZAJI WA NHC KUPITIA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maghala unaotekelezwa na S...