JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA
Msanii Juma Nature ‘Kiroboto’ akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said Christopher ‘Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri ‘Msagasumu’ na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix ‘Fredwayne’ Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher ‘Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
………………………………………………………………………………………………
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KOMAA CONCERT
Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya
msanii JUMA NATURE maarufu kama kiroboto pamoja na hitimisho la
sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA
CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi jumamosi hii ya tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar
Alive –Mbagala, kuanzia saa kumi na
mbili jioni.

Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana
na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa
93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka
kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo
Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Aidha, mashabiki watapata burudani kutoka kwa
kiroboto ambaye atatumia dakika 180
akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba
nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.
kiroboto ambaye atatumia dakika 180
akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba
nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.
Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu
na wengine wengi.
na wengine wengi.
Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm
Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata
burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.
Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata
burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.
Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji
kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi
kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza
muziki wa kizazi kipya.
kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi
kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza
muziki wa kizazi kipya.
Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza itaendelea
kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu sisi
tunaamini Muziki unaongea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu sisi
tunaamini Muziki unaongea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
IMETOLEWA NA, DENIS SSEBO,
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM.
Comments