Friday, May 22, 2015

NANI KUJINYAKULIA TUZO ZA FILAMU 2015 KESHO JUMAMOSI!

Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(katikati) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao katika ofisi zake kuelezea siku ya tuzo za filamu zitakazofanyika jumamosi hii jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Bwana Ezekiel kutoka Push Mobile na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa EATV na EAR Happy Shame.
 Meneja Masoko kutoka EATV na EA Radio Happy Shame(kulia)akielezea jambo kwa Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba wakati wa mkutano na wana habari kuhusu Tuzo za Filamu Tanzania 2015 leo jijini Dar es Salaam ambapo EATV na EAR ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo.

Mei 23, hapatoshi Mwalimu Nyerere Internnational Conference Center;

 Ni siku moja tu imebaki kufanyika kwa tuzo kubwa za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015(TAFA). Ni tuzo kubwa ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei 2015, Mwalimu Nyerere International Conference Center. Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini na kila mmoja ana shauku ya kushuhudia tuzo hizo zitakazo wapa wasanii wetu amsha amsha ya mafanikio katika tasnia yao.

Akiongea na wana habari katika ofisi zake raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba alisema, “Maandalizi yote yapo tayari na tumejipanga kikamilifu kufanikisha tuzo hizi. Kutakuwa na burudani mbalimbali kusherehesha tuzo hizi zikiongozwa na mzee Kikii, Mwasiti na Barnaba, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wana tasnia ya filamu watakaowakilisha vizuri kabisa tasnia yao kwa kutufanya tucheke na tufurahi. 

Yote hii ni kuwaburudisha wageni wetu watakaokuja kutuunga mkono katika siku hii muhimu kwa wana tasnia ya filamu.Tuna wageni mbalimbali ambao wameshafika kutoka nchi tofauti za Afrika ili kutuunga mkono katika hafla hii”.

 “Napenda kuwashukuru waisani mbalimbali waliojitolea kutuunga mkono Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani Production. Kwa namna ya pekee nashukuru vyombo vyote vya habari kwa sapoti kubwa waliotupa kipindi chote cha mchakato wa tuzo hizi tangu wakati wa uzinduzi hadi sasa bado wapo nasi bega kwa bega.”

“Wito wangu kwa watanzania na wana Afrika Mashariki kwa ujumla kutuunga mkono kwa kununua tiketi za hafla hii ili waweze kufika kushuhudia tuzo hizi za kipekee zitakazo andika historia mpya katika tasnia ya filamu. Tiketi zinapatikana kwa bei ya 50,000/= kawaida na VIP ni 100,000/= katika vituo vifuatavyo;Shear Illussion - Mlimani City and Millenium Towers, Robby One Fashion- Kinondoni and Sinza Africasana, B&B Boutique- Dar Free Market duka namba 46 na Viva Towers duka namba 31, Secky Bureau de Change - Big Bon Sinza Mori,  Save Mart wholesalers - Mikocheni kwa Nyerere EATV na ITV.  Karibuni sana tufurahie na kuunga mkono kazi za wasanii wetu.” Alisisitiza Mwakifwamba.

Tuzo za Filamu Tanzania 2015 zitakua na ‘surprises’ za kutosha hasa kushuhudia mastaa kutoka nchi za Ghana na Nigeria na mengine kibao. Watanzania wajitokeze kwa wingi kuunga mkono kazi za wasanii wetu hii ni kuonesha uzalendo kwa kupenda kazi za wasanii wetu.

No comments: