Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Wakurugenzi wa Shirika hilo wakishuhudia tukio la kuzinduliwa kwa tukio hilo
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Picha zaidi za tukio la uzinduzi huu tutawaleteeni baadaye.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU
UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU NA MALIPO YA KODI KWA
MFUMO WA SIMU ZA KIGANJANI – MEI 19, 2015
Katika jitihada za Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua
huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa
kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani.
1.
Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya
simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji
kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa
mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao. Wateja wataweza
kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki
Shirika linawaahidi kwamba maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa
kipaumbele kwa kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
2.
Katika kuendelea kuboresha mfumo wa
ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa
kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao
bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na airtel money. Kupitia mfumo
huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na wataweza
kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda Shirika la Nyumba
mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni muafaka kwao bila ya kufika
katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
No comments:
Post a Comment