WIZARA ITAPUNGUZA KWA ZAIDI YA NUSU GHARAMA ZA UPIMAJI ARDHI ILI KILA MWANANCHI AWEZE KUPIMA ENEO LAKE NA KUPATA HATI- MHE WILLIAM LUKUVI

1
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua
4
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
5
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.
……………………………………………………………
Na Clarence Nanyaro
Kuanzia mwaka ujao wa fedha,serikali itapunguza gharama mbalimbali za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwezesha wananchi wengi kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekithiri hapa nchini.
Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora,Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati suala ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inatokea.
Aidha Mh Lukuvi aliongeza kuwa sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi, serikali pia itaweza kukusanya bkwa wingi kodi ya pango la ardhi na hivyo kuongeza mapato amabayo yataisiaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo pamoja na kupunguza gharama hizo Wazrizi Lukuvi aliwaonya Maafisa ardhi,kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu,akitolea mfano wa maafisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Maafisa ardhi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao” alisema Mh Lukuvi na kuongeza kuwa atakayebainika kukiuka taratibu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.
Waziri Lukuvi yuko mkoani Tabora kwa shughuli za kikazi,ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa anatafuta suluhu ya migogoro ya ardhi katika manispaa ya Tabora ambapo alikutana na wananchi wa maeneo ya Malabi,Uledi,Malolo na Kizigo ambako kumekuwa na migogoro ya ardhi kutokana na baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kutolipwa fidia baada ya Manispaa ya Tabora kupima viwanja katika maeneo hayo.
Akiwa katika eneo la Malabi,Waziri Lukuvi aliiagiza Manispaa ya Tabora kupima upya eneo hilo na kulipatia kanisa la African Inland Church (AIC) ekari kumi na ekari 28 zipimwe kwa ajili ya Wananchi ili kumaliza mgogoro huo na kmujongeza kuwa kila atayepata hati lazima ahakikishe kuwa analipa kodi ya pango la ardhi.
Awali,Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua aliweleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa kwa sasa Mkoa wa Tabora ndio wenyewe eneo kubwa na hivyo juhudi na nguvu kubwa inatakiwa ili kupima maeneo mengi kuepusha migogor ya ardhi. Tayari Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeidhinisha shilingi milioni 142 kusaidia manispaa ya Tabora kupima maeneo yake.

Comments