MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TATU, NCHINI CHINA, AKUTANA NA MWENYEJI WAKE MAKAKU WA RAIS WA CHINA

gh1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili kwenye Ukumbi Maalum kwa watu wa China. ‘Peoples Great Hall’, jijini Beijing China kwa ajili ya mazungumzo rasmi, alipoalikwa kwenye chakula cha jioni na Makamu wa Rais wa China baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo. jana Mei 20, 2015. Picha na OMR
gh2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya China, wakati alipowasili kwenye ukumbu Maalum wa watu wa China, ‘Peoples Great Hall’ kwa ajili ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, jana Mei 20, 2015. Picha OMR
gh3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo. Picha na OMR
gh4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina. Picha na OMR
gh5gh7gh8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, ‘Peoples Great Hall’ baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR


gh9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisindikizwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Kushoto ni mkarimani wa Makamu wa Rais wa China. Picha na OMR
gh10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR
………………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Mei 20, 2015 amemalizia ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini China ambapo amekutana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China Mheshimiwa Li Yuanchao na kupata mapokezi Rasmi ya Serikali ya China katika ‘Ukumbi Maalum’ kwa wa Watu wa China. Makamu wa Rais katika mapokezi hayo alipata nafasi ya kukagua gwaride na kisha kuongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Yuanchao katika ukumbi wa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa China alitumia nafasi hiyo kumshukuru Makamu wa Rais wa Tanzania kwa kukubali mwaliko wake na hivyo kufanya ziara ya kikazi nchini China na pia akaongeza kuwa, uhusiano wa China na Tanzania ni wa wakati wote na akasisitiza kwamba ushirikiano baina ya nchi hizi mbili unatoka katika mioyo ya wananchi. “Nilipokuwa Tanzania mwaka jana mwezi wa Juni niliona namna raia wa China anavyothaminiwa na kuheshimiwa nchini Tanzania. Jambo hili lilinipa furaha na kunielimisha kuhusu nchi zetu,” Makamu wa Rais Yuanchao alisema.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal alitumia nafasi hiyo licha ya kushukuru kwa Mwaliko pia kuzungumzia agenda za maendeleo ya Tanzania huku akisisitiza kuwa, anayo furaha kuhusu kukamilika kwa usimikaji wa mkondo wa Taifa kwa awamu zote mbili huku akiitaka serikali ya China kuendelea kuwa na Tanzania katika kukamilisha awamu ya tatu, jambo ambalo Makamu wa Rais Yuanchao alilikubali.
Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alizungumzia pia ziara yake katika majiji ya Wuhan na Nanjing na akaelezea furaha yake kuhusu namna wananchi wa China wanavyoitazama Tanzania na namna walivyo tayari kushirikana nayo katika kukuza maendeleo ya viwanda sambamba na kutanua soko la biashara baina ya Tanzania na nchi zinazoizunguka. Pia alipata nafasi ya kuzungumzia kuhusu namna ya kuboresha reli ya TAZARA huku akimtaka Makamu wa Rais Yuanchao kusaidia kwa kuwaita Mawaziri wa Uchukuzi toka Zambia na Tanzania ili wakutane na wenzao wa China ili kuhakikisha kunapatikana mkakati mpya wa namna ya kuiendesha Reli hiyo kwa faida ya nchi washirika.
“Reli hii ni moja ya viashiria vikubwa vya historia ya mahusiano yetu. Sisi Tanzania tusingependa kuona inakufa,” alisema Makamu wa Rais Dkt. Bilal na kuongeza kuwa mazungumzo kama hayo yanatakiwa kufanyika katika mradi wa ujenzi wa sehemu ya uwanja wa ndege wa Zanzibar ambao umesimama ujenzi kufuatia pande mbili kushindwa kuelewana.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa China yeye aliihakikishia Tanzania kuwa China inao uzoefu mkubwa katika mambo mengi hivyo Tanzania inatakiwa kutumia urafiki wake na China katika kushirikiana kwenye masuala ya maendeleo. Pia alifafanua kuwa serikali za Tanzania, Oman na China zinatakiwa kuendelea kushirikana katika suala la Ujenzi wa Bandario na Bagamoyo na kwamba serikali yake imejipanga kuendelea kuwafadhili wanafunzi wa Kitanzania kusoma masomo ya Mafuta na Gesi.
“Wakati nilipokuwa Tanzania nilifurahishwa na namna watu wenu wanavyoonesha uwezo wa kukabiliana na changamoto za sasa. Watu hawa wanaweza kabisa kufanya kazi za aina mbalimbali hivyo sisi tunaitazama Tanzania kama sehemu ya kuifanya Afrika itanuke na hivyo uhusiano wa China na Afrika ubakie kama ulivyokuwa katika kipindi cha Afrika kutafuta uhuru,” alisema.
Mheshimiwa Makamu wa Rais amemaliza ziara yake na moja kwa moja kuanza safari ya kurejea nchini ambapo anategemea kushiriki mikutano ya Chama cha Mapinduzi inayofanyika mjini Dodoma. Katika ziara hiyo ya siku tatu nchini China, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal aliambatana na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna. Mwingine ni Naib u Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Mei 20, 2015
Beijing, China

Comments