Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yatoa Ratiba Rasmi ya Uchaguzi Mkuu.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian  Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Comments