Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana. Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho. Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro)
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na walimu waliofika katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea jijini Arusha .Jumla ya walimu 1000 wanahudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini. Picha na Mahmoud Ahmad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiteta jambo na mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho jijini Arusha.Jumla ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini.Picha na Mahmoud ahmad
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea jijini Arusha. Jumla ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo Rais Kikwete alihutubia. Picha na Mahmoud Ahmad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akizungumza jambo na mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho
Comments