Thursday, May 28, 2015

WAZIRI MAHENGE:ASILIMIA 61 YA ARDHI NCHINI IMEHARIBIKA, AIRTEL YAPIGA JEKI SIKU YA MAZINGIRA

ASILIMIA 61 ya ardhi nchini imeharibika kutokana uharibifu wa mazingira ya ardhi  katika vyanzo vya mbalimbali na kusababisha kuzama kwa baadhi ya viziwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Mhandisi Binith Mahenge wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani  yatakayofanyika Juni 5 mwaka  huu mkoani Tanga.  Mahenge amesema Juni 5 ya kila mwaka iliamuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 kuwa Siku ya mazingira duniani kutokana na kuonekana baadhi  ya vyanzo vinapotea kutokana na uchafuzi mazingira.

Amesema mikoa ambayo imekuwa kame kutokana na uharibifu wa mazingira ni Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida,Simiyu na Kilimanjaro huku kasi yaukataji miti ikiwa inaongezeka na kufikia hekta 400, 000  kupotea kila mwaka nchini. Waziri huyo ameunga mkono kwa Kampuni ya simu za mikononi Airtel kuungana kuadhimisha siku ya mazingira kwa kuchangia kutoa elimu kwa njia ujumbe mfupi.

Afisa Mawasiliano na Matukio wa Airtel,Dangio Kaniki,amesema watatoa
ujumbe mfupi kwa ajili ya kutoa elimu kwa katika kuhamasisha utuzaji
wa mazingira na kutaka makampuni mengine yajitokeze kuunga juhudu za
utuzaji wa mazingira. Dangio,amesema ujumbe mfupi wataotoa katika utuzaji wa mazingira katika maadhimisho hayo ni zaidi ya Sh.milioni 90 ambazo Airtelingepata kutokana na kutuma ujumbe huo.
 
  Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (katikati) akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (kushoto)akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa RaisDk. Julius Ningu msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel  Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayokitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika haflafupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni AfisaUhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto) na(kulia) ni Meneja Uthibiti wa Airtel, Calvin Simba
  Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (wa pili kulia)   akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhandisi Angelina Madete msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na (kulia) ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

No comments: