Kikao cha Kamati Kuu chaanza mjini Dodoma


 Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Mhe. Zakhia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu leo tarehe 22 Mei 2015 mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Jerry Slaa akishauriana jambo na Mhe.Wiliam Lukuvi ndani ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe wenzake wa Kamati Kuu Profesa Makame Mbarawa Mnya na Dk. Salim Ahmed Salim kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma wakijiandaa na kikao cha Kamati mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezu Nape Nnauye akisoma gazeti ndani ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wengine Abdala Bulembo na Hadija Aboud ikiwa sehemu ya kujiandaa na kikao cha Kamati Kuu kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Profesa Makame Mbarawa Mnya huku Dk. Salim Ahmed Salim akipitia baadhi ya makabrasha kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma wakijiandaa na kikao cha Kamati mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe.Adam Kimbisa akimsikiliza kwa makini mjumbe mwenzake Mhe.Stephen Wasira kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza ndani ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.

Comments