ENG. STELLA MANYANYA AONANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA JIANGXI KUTOKA CHINA INAYOJENGA BARABARA YA LAMI MKOANI RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia ofisini kwake Jana tarehe22/05/2015. Kampuni hiyo inajenga barabara ya lami kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi katika mradi wa Sumbawanga-Kanazi (KM 75). Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ushirikiano wake mzuri na uongozi wa Mkoa katika shughuli zake za ujenzi wa barabara hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akiongoza zoezi la utambulisho wa wageni na wenyeji katika kikao hicho.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia akizungumza katika kikao hicho ambapo ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano unaowapa katika kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami ya Sumbawanga – Kanazi, aliongeza kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya kazi zingine mbalimbali Mkoani Rukwa ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka pamoja na kuwekeza katika eneo la ufugaji.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya walipomtembelea Ofisini kwake leo. Barabara ya Lami ya Sumbawanga – Kanazi – Namanyere – Kizi – Kibaoni inajengwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania na ujenzi wake bado unaendelea.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua muda mfupi kabla ya kuagana Jana. Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
Comments