PSPF YAUNGANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KATIKA HAFLA YA KUENDELEZA UMOJA WA WAJASIRIAMALI DAR ES SALAAM
Meneja
msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu wa mfuko wa pensheni wa
(PSPF) akieleza namna ya mfuko wa Hiari unavyo kuwa na ni jinsi gani
utafaidika pindi unapo jiunga na kuwa mmoja wa wadau wa (PSPF)
Kushoto
Muandaaji wa sherehe ya wanawake wajasiliamali Shamimu Mwasha ambaye ni
mdau wa (PSPF) akitoa ufafanuzi wa sherehe hiyo na kuwakaribisha wageni
walioweza kuhudhuria pembeni ni mshereheshaji wa sherehe hiyo Jokate
Mwegelo.
Baadhi
ya wanawake wajasiriamali wakiwa wameketi pamoja huku wakiendelea
kupokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wanawake tofauti tofauti waliokuwepo
katika sherehe hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Wanawake
wajasiriamali Dar es salaam washerehekea pamoja katika hafra fupi iliyo
andaliwa na Mjasiriamali Shamimu Mwasha kwa lengo la kuendeleza kuwa na
mahusiano mazuri katika shughuli zao za kuijenga nchi kwakutumia
vipaji na ubunifu walionao ili kuhakikisha bidhaa mbalimbali
zakitanzania hazikosekani katika soko la hapa nyumbani hata nje ya nchi.
Mfuko
wa jamii wa (PSPF) umeweza kuwaunga mkono wajasiriamali hao kwa kuwa
miongoni mwa mfuko unaotoa huduma mbalimbali kupitia mafao yao kwakuwa
kunamafao mbalimbali katika mfuko wa pesheni ambayo wao kama
wajasiriamali wanaweza kuyamudu na hatimaye kufikia malengo waliyo
jiwekea.
Akizungumza
wakati wa sherehe hiyo Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda
Nyallu amesema mfuko wa jamii wa (pspf) ni mfuko unao jali kila mmoja na
nimfuko ambao unakupatia wewe mtanzania faida maradufu kutokana na
huduma zinazo tolewa kuwa za kiwango cha hali ya juu amesema kupitia
mafao mbalimbali likiwemo fao la mikopo ya elimu,fao la
ujasiriamali,nyumba na mengine mengi pia aliweza kuwaeleza kuhusu
uchangiaji wa hiari ambapo kupitia uchangiaji huo mtu yeyyote anaweza
akaumudu kutokana ni rahisi na inakiwango cha kawaida cha kuchangia .
Comments