UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

DSC_0281
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
DSC_0282
Sasa limezinduliwa rasmi.
DSC_0287
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0318
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
DSC_0340
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha “Ultra sound” kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0362
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
DSC_0373
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
DSC_0386
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
DSC_0388
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
DSC_0411
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
DSC_0421
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC pamoja na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.

Comments