Menyekiti wa chamacha wamiliki wa vyombo vya habari nchini, MOAT, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, (kushoto), akijadili jambo na Mkurugenzi wa New Habari 2006 Limited, Rostam Aziz, walipokutana kwenye kikao cha MOAT kujipanga na kujadili namna ya kukabiliana na mpango wa serikali wa kuwasilisha muswada wa habari kwa mara ya pili. Mkutano huo ulifanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na umeazimia kuunda timu ya watu watatu ambao watasafiri kwenda Dodoma, ili kukutana na kamati ya bunge ya katiba na sheria ili kuitaka kamati hiyo kuzuia serikali kuwasilisha muswada huo kwa mara ya pili. Duru za habari zinaeleza kuwa Muswada huo pamoja na mambo mengine, utalazimisha vituo vya runing vya kibinafsi, kujiunga na televisheni yha taifa (TBC) kwa taarifa ya habari ya saa mbili usiku (2;00), hatua ambayo inapingwa vikali na wamiliki wa vyombo binafsi ambao wanasema ni uonevu katika ushindani huru hususan ikizingatiwa TBC ambayo ni televisheni ya Watanzania wote kupitia kodi wanazolipa, nayo "inagombea" matangazo ya biashara kama vyombo binafsi
|
Dkt. Mengi, Tido Muhando, kutoka Azam TV, (katikati) na mkurugenzi wa Mwanachi Communications Limited, Francis Nanai |
|
Kutoka kushoto, Rostam Aziz, Dkt. Mengi, Godfrey Mpandimizi, mwanasheria kutoka LHRC, na Mkurugenzi wa Sahara Media Group, Samwel Nyalla |
|
Mpandimizi, Nyalla, na Mkurugenzi wa Hali Halisi, Saed Kubenea |
PICHA ZOTE ZA KHALFAN SAID
Comments