Wednesday, May 20, 2015

MAFUNZO YA PROGRAMU YA AWAMU YA PILI YA KUBORESHA TAALUMA YA WALIMU NA WANAFUNZI YAZINDULIWA WILAYANI SAME


 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela akizungumza na walimu (hawapo pichani) waliohuduria mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania na Mratibu wa Basic Support Program Julius Lugemalila akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same. 
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Elimu ya msingi TAMISEMI Kassim Kaoneka akiongea na naibu Wazirir wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ,viongozi wa elimu na walimu walioshiriki mafunzo ya Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.
 Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Same walioshiriki mafunzo ya  Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same. 
Mwalimu Ruth Elifuraha akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anne Kilango Malecela amewataka walimu wanaofanya kazi katika maeneo wanayotoka kuwa na nidhamu ya kazi ili kuendelea kuinua ubora wa Elimu nchini. 

Akizungumza katika uzinduzi wa Programu ya awamu ya pili ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi inayoendelea katika wilaya ya Same amesema sababu kubwa ya kushuka kwa taaluma katika wilaya hiyo ni kutokana na walimu kufundisha katika maeneo ya nyumbani. Kitu kinachosababisha  muda mwingi kushughulikia matatizo ya familia zaidi. 

"Walimu wanaofundisha maeneo ya nyumbani mara nyingi hukosa nidhamu ya kazi kwa kutofanya kazi uadilifu na badala yake kuishia kutatua matatizo yanayozunguka ndugu na jamaa" alisema Naibu Waziri.Aidha, amewataka kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanawatendea haki watoto wanaowafundisha na kuheshimu muda wa serikali kwa kufanya kazi kwa masaa wanayopaswa kufanya kazi.

 Serikali ilianzisha Programu ya kuboresha taaluma ya walimu na wanafunzi ili kukabiliana na changamoto za kushuka kwa kiwango cha ufaulu. Programu hii iitwayo Programu ya Mafunzo ya Kujenga Uwezo kwa Walimu na Wanafunzi katika ujifunzaji na ufundishaji inalenga kuongeza kiwango cha ufaulu.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi ngazi ya shule  yanasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Srikali za Mitaa (TAMISEMI). Ufuatiliaji wa mafunzo unafanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 

Baada ya mafunzo haya walimu wanapaswa kuanzisha madarasa rekebishi ili kuinua kiwango cha taaluma na ufaulu kwa wanafunzi kulingana na mazingira yao.   

No comments: