Tuesday, May 12, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI KLABU ZALENDO KATIKA MANISPAA YA LINDI

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kwa kuyapungia mkono maandamano ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Lindi ambao ni wanachama wa Klabu Zalendo wakiongozwa na chipukizi kwenye Uwanja wa Ilulu wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa klabu hiyo tarehe 10.5.2015.
11
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Klabu Zalendo iliyoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwenye Uwanja wa Ilulu tarehe 10.5.2015.  Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bwana Yahaya Nawanda na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu Zalendo Mwalimu Mwajuma Malugu.
23
Vijana wa chipukizi kutoka Klabu Zalendo katika Manispaa ya Lindi wakionyesha michezo ya halaiki wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa klabu yao uliofanywa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye uwanja wa Ilulu tarehe 10.5.2015.
4
Vijana wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule za Msingi katika Manispaa ya Lindi wakishiriki kwenye riadha kwa kukimbia mbio za mita 100 wakati wa sherehe za uzinduzi wa Klabu Zalendo.
8
7
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wanachama wa Klabu Zalendo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kucheza wimbo wa ‘NANI KAMA MAMA’ muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi klabu hiyo inayoundwa na walimu, wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja wa wananchi mbalimbali katika Manispaa hiyo.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments:

KIPANGULA: WAHITIMU WA HABARI WATAFAIDIKA NA MABORESHO YA KANUNI

  Na Mwandishi Wetu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amewashauri Waandishi ...