Wednesday, April 01, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AHITIMISHA ZIARA YAKE YA MIKOA MITATU MKOANI KILIMANJARO.


Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili Moshi Mjini kutokea Wilaya ya Rombo kwa Ziara ya siku kumi  ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wamekamilisha ziara yao ya mikoa mitatu ikiwemo Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, Ziara hiyo ililenga Kuimarisha, kutekeleza na kuhimiza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CCM, ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
wananchi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye huku wameweka mikono kichwani kuashiria kuwa miaka 20 kwa upinzani jimbo la  Moshi mjini imetosha.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.
Wakazi wa Moshi mjini wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia,ambapo aliwaeleza kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM kuongoza mji wa Moshi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
Jengo la soko la kati Moshi mjini likiwa liemacha kama pagala baada ya wafanyabiashara wa soko hili kuondolewa na kuachwa kama lilivyo mpaka sasa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajiri na kutambulika na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.

No comments: