Monday, April 13, 2015

18 WAPOTEZA MAISHA, 11 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA NGANGA NA FUSO MKOANI MOROGORO

Na Father Kidevu Blog, Morogoro.
WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine  11  wakijeruhiwa vibaya  kwa moto kufuatia magari mawili kugongana ambayo ni Basi Scania mali ya kampuni ya Nganga lililosajiliwa kwa namba T373 DAH  na gari ;la mizigo Mistubishi Fuso T164 BKG.
Ajali hiyo imeelezwa kutokea majira ya asubuhi saa mbili katika Kijiji  cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Polisi mkoani Morogoro kupitia kwa Kamanda wake, Leonald Paulo imesema
 chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo
 kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha  ajali hiyo.
Kamanda Paulo aksema basi lilikuwa limepakia pikipiki katika buti na ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basin a lori hilo.
Mbali na abiria waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa na majeruhi takribani 11 walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito  Mikumi.

No comments:

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...