Friday, June 26, 2026

RAIS SAMIA APONGEZA MPANGO WA HEIDELBERG MATERIALS KUPANUA UWEKEZAJI NCHINI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea ujumbe wa Kampuni ya Heidelberg Materials, wazalishaji wa saruji za Simba Cement na Twiga Cement, ulioongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Uongozi na Mtendaji Mkuu wa Afrika, Mediterranean na Asia Magharibi, Bw. Hakan Gurdal, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, tarehe 26 Juni 2026.

Katika kikao hicho, Heidelberg Materials imewasilisha mpango wake wa kupanua uwekezaji nchini Tanzania, ukiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa saruji ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya sekta ya ujenzi na miundombinu.

Mbali na kuongeza uwezo wa uzalishaji, kampuni hiyo imeeleza dhamira ya kuwekeza zaidi katika matumizi ya nishati safi pamoja na kutekeleza mradi wa usindikaji wa taka za majiji kwa ajili ya uzalishaji, hatua inayolenga kuimarisha ulinzi wa mazingira na kuchochea maendeleo ya uchumi wa kijani.

Mpango huo unatarajiwa kuimarisha sekta ya ujenzi, kuongeza ajira, kukuza shughuli za viwanda na kuendelea kuiweka Tanzania kuwa kitovu muhimu cha uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hatua hiyo inaendana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuvutia uwekezaji wenye tija, kuongeza thamani ya rasilimali za nchi na kuharakisha maendeleo ya uchumi kupitia sekta ya viwanda.


No comments:

RAIS SAMIA APONGEZA MPANGO WA HEIDELBERG MATERIALS KUPANUA UWEKEZAJI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea ujumbe wa Kampuni ya Heidelberg Materials, wazalishaj...