Monday, March 03, 2014

Jionee Mwenyewe Picha Mbalimbali Jinsi mashabiki wa timu ya soka ya Simba ambayo ni wapinzani wa jadi wa Yanga, walivyoanza kung'oa viti na kuvirusha upande walipokuwa wameketi washabiki wa Yanga

 
Jana  katika Mchezo wa soka wa kinyang'anyiro cha klabu bingwa Barani Afrika, uliozikutanisha timu za Yanga (Tanzania) na Al-Alhly (Misri) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (Tanzania), timu ya Yanga imepata ushindi wa goli moja.


Lakini cha kustajaabisha ni ripoti kuwa kabla hata ya kuanza kwa mtanange huo, baadhi ya mashabiki wa timu ya soka ya Simba ambayo ni wapinzani wa jadi wa Yanga, walianza kung'oa viti na kuvirusha upande walipokuwa wameketi washabiki wa Yanga. 



Chokochoko  hizo inaripotiwa kuwa zilitulia wakati mchezo ukiendelea, ila zikarejea tena mara baada ya Yanga kupata goli, saari hii ni mashabiki wa Simba tena waliovalia jezi za Simba walianza tena kung'oa viti na kuwarushia mashabiki wa timu ya Yanga waliokuwa wakishangilia. Tizama picha zaidi hapo chini.

No comments:

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...