Wednesday, March 05, 2014

LG YAZINDUA JOKOFU LENYE UWEZO WA KUTUNZA UBARIDI KWA MUDA WA MASAA 7‏

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania, Mayur Parikh ambao ni wasambazaji bidhaa za LG, akiwa na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) pamoja na mfanyakazi wa kampuni hiyo wakizindua jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi ubaridi kwa muda mrefu. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Zoezi la kuzindua likiwa…
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania, Mayur Parikh ambao ni wasambazaji bidhaa za LG, akiwa na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) pamoja na mfanyakazi wa kampuni hiyo wakizindua jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi ubaridi kwa muda mrefu. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Zoezi la kuzindua likiwa limekamilika.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania, Mayur Parikh ambao ni wasambazaji bidhaa za LG, akifungua jokofu hilo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia).
 Afisa Masoko wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania ambao ni wasambazaji wa Bidhaa za LG, Grace Kavishe, Carolyn Jesse akiongea na waandishi wa habari kuwaelezea jinsi jokofu hilo linavyoweza kufanya kazi.
 Muonekano wa jokofu hilo kwa ndani.
 Akiendelea kuelezea ubora wa jokovu.
 Mwakilishi wa kampuni ya LG Tanzania, Carolyne Yesse akitoa maelezo.
 Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania, Mayur Parikh.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania, Mayur Parikh akitoa malezo ya awali.
---
Kampuni ya vifaa vya Umeme ya LG leo imezindua jokofu la kisasa zaidi yenye uwezo wa kutunza ubaridi kwa muda wa masaa saba upande wa jokofu ya kawaida na masaa kumi kwa upande wa friza hata pindi umeme unapokuwa umekatika.

Bidhaa hii mpya imezinduliwa mahususi kutokana na tatizo lililo kithiri la katizo la umeme ambalo hukumba maeneo mengi ya nchi na kusababisha vifaa vya umeme kukosa matumizi kwa muda mrefu.

Aidha tatizo hili la kukatika kwa umeme mara kwa mara kumepelekea makapuni kama LG kutanua wigo wao katika kutafuta suluhu na hivyo kubuni teknolojia zenye usasa uliopindukia katika ubunifu wa vifaa vitavyo himili nyakati umeme unapokosekana. Ni katika ubunifu huo ndipo LG ikatengeneza jokofu hili jipya lisilogandisha barafu kwenye “friza” linaloweza kutunza ubaridi katika sehemu ya ‘friji” kwa zaidi ya masaa saba hasa pale umeme unapokatika kwa kipindi kirefu.
Akiongea siku ya uzinduzi Appliances Product Manager LG East Africa, Oktae Kim alisema uzinduzi huu umelenga katika ubunifu mkubwa unaohusiana na mahitaji ya mteja na jinsi ya kuyatatua. Hivyo basi tunajitahidi kubuni bidhaa ambazo zina kidhi mahitaji ya wateja wetu.

Teknolojia iliyotumika inahusianisha valve kwenye jokofu ambayo hufunguka pale ambapo kunapokosekana na umeme. Valve hii inasambaza ubaridi kwenye vifaa vingine vilivyoundwa maalumu kutunda ubaridi na pindi umeme ukatikapo vipaa hivi huanza kutoa ubaridi kwa muda wa saa saba.
Bwana Kim amesema: “Evercool inapooza mara tatu zaidi kwa kutumia evaporator tatu.
Evaporator kuu inatumia umeme na mbili zinafanya kazi bila kutumia umeme. Kwa hiyo sasa unaweza kufaidi vinywaji baridi na kuepuka kuharibika kwa chakula chako kwenye jokofu mara umeme unapokatika”.

LG ina visahani vya kugandishia barafu ambavyo vina uwezo wa kugandisha barafu kwa haraka ya zaid ya asilimia 20. Imetengenezwa kwa umahiri na maeneo ya kutosha kwa ndani na hivyo kukuwezesha kupata sehemu ya kutosha ndani wakati wa kuweka vitu. Sasa unaweza kutunza mboga na matunda vizuri bila kuogopa vitu kuharibika kutokana na mrudikano wa vitu nahivyo kusababisha unyevunyevu unaopelekea kuharibu vyakula.
Na wakati wa kipindi cha joto kali, jokofu hili la milango miwili litakushangaza kwa kutunza chakula kwa hali ya juu.
Pia mwanga wa LED unang’aa zaidi, unadumu kwa muda mrefu na unatumia umeme mdogo. Na mtu atakayenunua jokofu hili hahitaji kutafuta ‘Stabilizer” kwani jokofu hili linaweza kufanya kazi vizuri hata wakati umeme unapokuwa mdogo.

Bw. Kim aliongezea kwakusema :compressor za LG ni Imara na tunakupa guarantee ya mwaka mzima” Pia aliongeza kuwa wanajitahidi kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa za kisasa na zinazoendana na mahitaji halisi ya watu.

No comments: