Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Matuli kata ya Chalinze kwa ajili ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akifurahia ngoma iliyokuwa ikitumbuizwa na kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chahua kata ya huko Bwiligu kwa ajili ya mkutano wa kampeni.Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akishiriki kucheza muziki wakati mwimbaji Hafsa Kazinja alipokuwa akitumuiza katika kijiji cha Matuli kata ya Chalinze .Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akifungua tawi la Msimamo Kijiji cha Chahua, kulia ni Mzee Kazidi Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa kampeni katika jimbo la Chalinze.Msanii Sam wa Ukweli akitumbuiza katika mkutano wa kampeni kijiji cha Matuli.Msanii Dokii akinengua huku morani wa kimasai wakimshangaa.Mzee Kazidi Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa kampeni katika jimbo la Chalinze akizungumza na MNEC Martin Shigela wakati mkutano huo wa kampeni ukiendelea.MNEC Martin Shigela akishiriki kucheza ngoma ya Kikwere wakati mkutano huo wa kampeniMsanii Dokii akishiriki kucheza ngoma iliyotumbuizwa na akina mama wa Kimasai katika mkutano huo wa kampeni.Morani wa Kimasai wakishiriki kwa makini katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matuli.Baadhi ya wananchi waliokampeni.hudhuria katika mkutano huio wa MNEC Martin Shigela akiwahutubia wananchi wakati mkutano huo wa kampeni.
Comments