Thursday, March 20, 2014

MKUTANO WA DIASPORA NCHINI UINGEREZA 2014

KAMATI YA MAANDALIZI YA
MKUTANO WA DIASPORA NCHINI UINGEREZA 2014
Kufuatia hatua ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kuunda kamati ya muda (Tanzania UK Diaspora Task Force) itakayosimamia maandalizi ya Mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014, tunapenda kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati hiyo kwa Watanzania waishio Uingereza.
Kamati hiyo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga akisaidiwa na Bw. Cleopa John katika nafasi ya Katibu. Aidha Bi Maxine Brown atashughulikia mawasiliano kati ya kamati na watanzania waishio nchini Uingereza.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni wafuatao:
Salim Amar: Makamu Mwenyekiti
Mariam Mungula: Makamu Katibu
Hassan Mussa: Mratibu wa Wajumbe wa Kamati
Mchungaji Mathew Jutta: Mjumbe
Kassim Kalinga: Mjumbe
Amos Msanjila: Mjumbe
Allen Kuzilwa: Mjumbe
Sheikh Rashid Saleh: Mjumbe
Watanzania waishio Uingereza mnaombwa kuunga mkono uongozi wa kamati  hii katika kufanikisha mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014. Kwa kuanzia Watanzania mnaweza kutuma maoni kuhusu mnayotarajia kuyaona kwenye  Mkutano wa Diaspora mwaka 2014 kwa kujaza fomu ya utafiti iliyopo kwenye anuani ifuatayo : https://www.surveymonkey.com/s/5VVGK9Z
Aidha mawasiliano na Kamati yanaweza kufanyika kupitia mitandao ya kijamii ifuatayo:
Twitter: @tanzaniaukdiasp

No comments: