Monday, March 31, 2014

WAZIRI MKUU PINDA AKABIDHI TUZO YA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14, DK MARIA KAMM AIBUKA SHUJAA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali yaMwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria…
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali yaMwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Dk. Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango MalecelaDk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo, akitoa hotuba fupi wakati wa utoaji tuzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kabla ya kukabidhi tuzo.
Dk. Maria Kamm na mumewe wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Pinda.
Anne Kilango Malecela na mumewe Mzee John Samuel Malecelawakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakiimba Wimbo wa Taifa.
Mama Magreth Sitta (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kulia) wakifuatilia zoezi la utoaji tuzo.
Dk. Kamm na mumewe wakiangalia Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Shigongo na Waziri Mkuu wakiteta jambo.
Profesa Tibaijuka akisalimiana na Mama Anne Kilango.
Dk. Kamm akisakata rhumba na Profesa Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiongea jambo na mume wa Dk. Kamm. Kushoto ni Dk. Maria Kamm.
Dk. Maria Kamm akitoa hotuba iliyovuta hisia za watu.
Shigongo akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu akiingia ukumbini kwa shangwe.
Shigongo akiwaongoza Mzee Malecela na mkewe Anne Kilango kuingia ukumbini.
Dk. Kamm akisalimiana na mwanafunzi wake, Anne Kilango.
Shigongo akiambatana na Anna Abdallah kuingia ukumbini.
Anna Abdallah akisalimiana na Prof. Tibaijuka.
DK. Maria Kamm ametwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 baada ya kuwapiku wenzake watatu jana usiku.
Dk. Kamm ametwaa tuzo hiyo baada ya kupata asilimia 32.5 ya kura zote zilizopigwa kupitia tovuti yawww.globalpublishers.info pamoja na meseji kupitia simu za mikononi.
Mshindi wa pili alikuwa Dk. Asha-Rose Migiro aliyejizolea jumla ya asilimia 30 ya kura zote, wa tatu Profesa Anna Tibaijuka akiwa na asilimia 20 na wa nne Anne Kilango Malecela mwenye asilimia 17.5 ya kura zilizopigwa kwa wanawake hao wanne walioingia Nne Bora.
Washidi wote wanne walipewa tuzo japo mshindi wa kwanza alijipatia medali pamoja na shilingi milioni tano.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Mkoani Dodoma, Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda aliyetoa tuzo hizo.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL, DODOMA)

No comments: