OLE SENDEKA, LEKULE LAIZA WAMFAGILIA RIDHIWANI KIKWETE CHALINZE,WAWATAKA WANACHALINZE WAMCHAGUE RIDHIWANI
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka akiwaomba Wananchi wa Lugoba,Jimbo la Chalinze kutofanya makosa kwenye Uchaguzi Mdogo ndani ya Jimbo lao na Wampigie Kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete. Sendeka aliyasema hayo jana Machi 17,2014 katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoni wakati alipopita kuwasalimia WanaChalinze.
Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh. Lekule Laiza akiwasalimia Wana Chalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
Comments