TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZWAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA MWONGOZO HOUSING ESTATE ULIOPO, KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Susan Omari,akizungumza na waandishi wa habari kaatika hafla ya uzinduzi wa nyumba za shirika hilo za Mradi wa Mwongozo Housing Edtate Uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika Makamo Makuu Mapya ya Shirika hilo  yaliyopoa katika makutano ya barabara za Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi mpya za shirika hilo zilizopo jijini Dar es Salaam, kuhusu uuzwaji wa nyumba za shirika hilo katika mradi wa Mwongozo zilizopo Kigamboni Dar es Salaam.(kushoto) ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo Tuntufye Mwambusi.


Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi mpya za shirika hilo zilizopo jijini Dar es Salaam, kuhusu uuzwaji wa nyumba za shirika hilo katika mradi wa Mwongozo zilizopo Kigamboni Dar es Salaam.(kushoto) ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo Tuntufye Mwambusi na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma za Jamii, Susan Omari. 

 Wanahabari wakimsikiliza mkurugenzi huyo.


Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), David Shambwe, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi mpya za shirika hilo zilizopo jijini Dar es Salaam, kuhusu uuzwaji wa nyumba za shirika hilo katika mradi wa Mwongozo zilizopo Kigamboni Dar es Salaam.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma za Jamii, SusanOmari.
 Wanahabari wakimsikiliza kwa makini alipokuwa akizungumzi uuzwaji huo.
 Waandishi wakiwajibika
 Baada ya mkutano walipata kifungua kinywa
 Wakipata kifungua kinywa baada ya mkutano.
Susan Omari, akiwa katika mazungumzo na waandishi hao wakati wa vitafunwa.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mwongozo zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu, kulia kwake ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Tuntufye Mwambusi na kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa nyumba za kuuza za makazi za Mwongozo zilizopo jijini Dar es Salaam leo mchana huu, kulia kwake ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Tuntufye Mwambusi na kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
sehemu ya umati wa waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo na waandishi wa habari.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZWAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA MWONGOZO HOUSING ESTATE ULIOPO, KIGAMBONI, DAR ES SALAAM


Kwa mara nyingine tena leo Jumanne, Machi 25, 2014 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linayo furaha ya kuwatangazia rasmi Watanzania wote mauzo ya nyumba 214 zinazojengwa eneo la Mwongozo, Kigamboni Jijini Dar es salaam.  

Taarifa hii ni ya uzinduzi rasmi wa nyumba takriban 214 zilizopo kwenye mradi wa Mwongozo Housing Estates ulioko karibu kabisa na bahari ya Hindi kilomita 19.5 kutoka kivuko cha Kigamboni, eneo la Mradi likiwa limepakana kwa karibu kabisa na Bahari ya Hindi. Uzinduzi wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Shirika la Nyumba la Taifa kukamilisha nyumba elfu 15,000 ifikapo mwaka 2015. Nyumba hizi tunazotangaza hii leo ziko za aina TANO zinazolenga kukidhi mahitaji ya wananchi  mbalimbali wenye uwezo wa kulipa kuanzia kiasi cha shilingi millioni 44.75/= mpaka millioni 128.9/= bila VAT ili kuwawezesha kila mwananchi kuwa na uchaguzi mpana kulingana na uwezo wake.

Tungependa kuwajulisha watanzania kuwa uzinduzi wa mauzo ya nyumba  hizi hii leo unawapa fursa ya kujiandaa kwa takribani wiki tatu kutafuta fedha za kununulia ili ifikapo tarehe 16 Aprili, 2014 waanze kulipia nyumba hizo. Hivyo, tunawakaribisha  watanzania wenye nia ya kununua nyumba za mradi huo kuwa ifikapo tarehe hiyo waanze kulipia  asilimia kumi kama malipo ya awali na baadaye wamalizie ili waweza kupata fursa ya kuwa wamiliki wa nyumba hizo bora na za kisasa kabisa zinazojengwa na Shirika.

Mradi huu wa mwongozo wenye nyumba za gharama nafuu unauzwa kwa kauli mbiu ya “Nyumba Yangu Maisha Yangu”, Miradi mingine ya aina hii ambayo bei ya nyumba zake zinaanzia shilingi milioni 36, inaendelea kukamilishwa ujenzi wake katika Halmashauri 14 za Wilaya hapa nchini. Maeneo hayo ni pamoja na Mvomero Morogoro, Mrara Babati, Mkuzo Songea, Bombambili Geita, Mtanda Lindi, Mlole Kigoma na Ilembo Katavi. Mingine ni Unyankumi Singida, Mkinga Tanga, Kongwa Dodoma, Longido Arusha, Kibada I Dar es  salaam na Uyui Tabora.


Mwongozo Housing Estate imejengwa na kujitosheleza kwa huduma zake za msingi kama zahanati, shule ya chekechea na maduka kwa ajili ya wakazi wake. Mradi wa Mwongozo Housing Estate unatarajiwa kuchukua wakazi zaidi ya 1,000 kupitia nyumba 214 zinazouzwa.

Nyumba za Mwongozo Housing Estate zimetenganishwa sehemu mbili za familia tofauti, moja ikiwa na vyumba viwili vya kulala na nyingine ikiwa na vyumba vitatu vya kulala, jiko la kisasa, sebule kubwa na mahali pa kula. Pia kila nyumba inayojitegemea na ina eneo kubwa la maegesho ya magari. Nyumba  zinajengwa kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa ili kumuwezesha mnunuzi kufurahia maisha ndani ya nyumba ya kisasa.
Tunawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wote walio nchini na walio nje ya nchi wafanye mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika, ofisi zetu za mikoa au kupitia baruapepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua nyumba katika mradi huu, tafadhali waweza tumia akaunti nambari:- 01J005161300,CRDB Vijana Branch au wasiliana na kitengo cha mauzo simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya shirika www.nhctz.com  kwa maelezo zaidi.
Aidha, tunapenda kuwafahamisha watanzania kuwa ahadi ya Shirika ya kujenga nyumba 15,000 kufikia mwaka 2015 inaenda vizuri na kwamba tuna imani kubwa kuvuka lengo hilo kwani hivi sasa miradi mbalimbali ya nyumba watu wenye kipato cha chini, kati na juu inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.


BW. DAVID SHAMBWE
MKURUGENZI WA UENDELEZAJI BIASHARA

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Comments