Tuesday, March 04, 2014

Picha Mbalimbali Kutoka Bunge Maalum La Katiba Mjini Dodoma


 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge  mjini Dodoma Machi 3, 2014 baada ya kusitishwa shughuli za Bunge Maalum  la Katiba.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta  na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,  Bungeni mjini Dodoma Machi 3,2014. Kushoto ni Kingunge Ngombale-Mwiru, Kulia ni Freeman Mbowe na Wapili kulia ni James Mbatia.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiwaeleza jambo Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya (katikati) na Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi(Kushoto).Wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Self Idd
 Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia akitoa mapendekezo juu ya taratibu za kupiga kura katika kufanya marekesho ya kanuni zitakazotumika katika Bunge Maalum la Katiba, wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akitoa mapendekezo yake kuhusu taratibu za upigaji kura unaoangalia maridhiano ya misingi ya kidemokrasia .Kulia ni Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum Prof. Mark Mwandosya na mbele ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa.wakati wa Semina ya Kujadili kanuni zaitakazoongoza Bunge Maalum la Katibaleo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia na Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi Charles Tizeba wakiwasili katika ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Pandu Ameir Kificho akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba alipowasili katika ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma kushoto kwake ni Bw. Mohamed Mbwana, katikati ni Rufai said Rufai na Kulia kwa Mwenyekiti ni Bw. Heri Khatibu.Picha na  Hassan Silayo-Maelezo na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments: