Thursday, March 13, 2014

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE (CUF) AMUWEKEA PINGAMIZI WA CHADEMA

TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF 
 DHIDI YA 
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA
13.03.2014
Mimi  FABIAN L. SKAUKI, Mgombea Ubunge wa Uchaguzi mdogo Jimbo la CHALINZE kwa tiketi ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo:
1.    Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza taarifa za uongo kwenye fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
2.    Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza  katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
3.    Ndugu MATHAYO M. TORONGEY  amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini, ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
4.    Ndugu MATHAYO M. TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa Jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni:
JINA LA MDHAMINI                                                            NAMBA YA KADI KURA

1.    HABIBU ALLY SAIDI                                                     *16886275*
2.    MOHAMMED RAMADHANI                                       *30376567*
3.    ABDULKADIR ALLY                                                      *49264905*
4.    SHABANI SULEYMAN                                                  *16984045*
5.    JUMA MRISHO                                                            *48759563*
6.    RAJABU ALLY                                                              *16872368*
7.    MANENO MIRAJI                                                        *16872059*
Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.
5.    Ndugu MATHAYO M. TORONGEY  amedanganya uraia wake na  kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.
Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ndugu MATHAYO M. TORONGEY  kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.
Wako katika ujenzi wa taifa,
FABIAN LEONARD SKAUKI
……………………………………………………..
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.
THE CIVIC UNITED FRONT
+255 786 189 070/+255 754 849 450

No comments: