Grace Tendega Mvandana Kampeni Meneja Wake ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Wakagua Vituo vya Kupigia Kura Kwa Helikopta
Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe(hayupo Pichani)namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akimjulia hali na kumsikiliza Mbunge wa Viti Maalum-Chadema, Rose Kamili akiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo mbunge huyo alimwelezea kiongozi huyo namna alivyotekwa, kuteswa na watu aliodai kuwa ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha Chama Ch Mapinduzi (CCM), Green Guard.
Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee, namna ambavyo Mbunge Rose Kamili alikuwa akiendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.
Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili lililotokea jana usiku katika Kijiji cha Kitawaya, Kaa ya Luhota, jimboni Kalenga, wakati alipokuwa akizungumza na mawakala wa CHADEMA, ambapo imedaiwa kitendo hicho kilifanywa na vijana wa ulinzi wa CCM.
Helikopya ya Chadema iliyowabeba Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akiwa na Kampeni Meneja wake, Godbless Lema akitua ambapo Godbless Lema na Grace Tendega walikua wakizunguka katika maeneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea jana.
Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akiwa na Kampeni Meneja wake, Godbless Lema muda mfupi baada ya kushuka kwenye helikopta yao walipokuwa wakizunguka katika ameneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea jana
Mgombea wa CHADEMA, Grace Tendega Mvanda akibadilishana mawazo na muda mfupi baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kuangalia shughuli ya upigaji kura vituoni ilivyokuwa ikiendelea leo.Picha Zote na Chadema
Comments