Monday, March 10, 2014

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete Atoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha maafa meja Jenerali Bakari Shaabani


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani huko Ada Estate jijini Dar es Salaam jana. Marehemu amezikwa nyumbani kwao huko Unguja Zanzibar Jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha maafa meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda Zanzibar na kuzikwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha Maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments: