RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA YA NJE WA UJERUMANI DKT FRANK-WALTER STEIMEIER IKULU

IMG_0083IMG_0085Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu kwa mazungumzo  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier. Waziri huyo aliwasili nchini tarehe 25.3.2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.IMG_0088Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na baadhi  ya viongozi aliofuatana nao wakati walipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014.IMG_0127 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmon na  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.IMG_0137Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonyesha wageni wake jengo la ikulu sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani) mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

Comments