Tuesday, March 19, 2013

Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare alipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, akionyesha vidole viwili huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wakati alipofikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana nyuma yake ambae nae amenyosha vidole viwili juu ni Joseph Ludovic Rwezaura wote kwa pamoja wamefunguliwa Mashtaka
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, akionyesha vidole viwili akiwa na Joseph Ludovic Rwezaura(Mwenye Flana ya Mistari) wote kwa pamoja wamefunguliwa Mashtaka
 Sehemu ya Wafuasi wa Chadema Walifika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Willfred Lwakatare (wapili kulia) na Ludovick Rwezahura (kulia) wakiondolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na askari kuelekea kupanda gari kwa ajili ya kurudishwa rumande, Dar es Salaam, jana.
Mbunge wa Singida Magharibi-Chadema  na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu(Kulia)akijadiliana Jambo na Mbunge wa Arusha Mjini_Chadema Godless Lema (Mwenye Shati Jeupe Kati)Nyuma Mwenye Shati la Mistari ni Vicent Nyerere Mbunge wa Chadema Musoma Mjini.Picha na Chadema na Mdau Michaeal Jamson 
----
Dar es Salaam. Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Rwezaura wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu waki kabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ong’o katika wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Msacky, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea........>>>>>

No comments: