ODINGA AKUBALI KUSHINDWA, ATAKA AMANI IDUMU KENYA

Rais wa awamu ya nne wa Kenya Uhuru Kenyatta, (kushoto) akijadiri jaambo na mpinzani wake Raila OdingaPresident elect Hon Uhuru Kenyatta addresses a press conference after the Supreme Court upheld IEBC declaration as the duly elected president.
President elect Hon Uhuru Kenyatta addresses a press conference after the Supreme Court upheld IEBC declaration as the duly elected president.  NATION MEDIA GROUP
 


 
MGOMBEA wa Urais nchini Kenya kwa tiketi ya muungano wa Chama cha CORD Raila Amolo Odinga amekubali kushindwa katika kesi ya kupinga matokeo aliyofungua katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Akihutubia taifa hilo muda mfupi uliopita,Odinga alisema kwamba anakubalina na uhumu hiyo iliyosomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga.

"Nimekubalina na matokeo hayo kwa sababu yakuheshimu Katiba ya Kenya ambayo inasema matokeo ya urais yapingwe katika Mahakama hiyo na maamuzi yatakayotolewa na Mahakama ndiyo ya mwisho"alisema Odiga.

Alisema, "Nilikwenda mahakamani kwa maslahi ya wakenya, hivyo natangaza rasmi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na kuitakia amani serikali iliyoko madarakani,nitashikiana nao katika kujenga nchi yetu".

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga kutoa hukumu ya kesi hiyo na kusema kwamba mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa huru na uwazi na kumfanya  Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto kuchaguliwa kihalali.

 hi yetu".

Comments