Mwandaaji
wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions
Blog, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama
Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake
wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo
kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea
kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani
kote.
Mgeni
Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya
wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla ya wanawake (Women's
Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions
Blog,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini
dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya
Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
Mwanamuziki
mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya
wageni waliohudhuria hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013)
iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions Blog,iliofanyika jioni ya leo
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.
Mke wa waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (pichani katikati) akijimwaya mwaya pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Naibu
Waziri wa Sheria na katiba,Mh. Angellah Kairuki akiwa sambamba na Mke
wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa wakifuatilia kwa makini
yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Mmoja wa washiriki wa hafla hiyo akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakifutailia mambo yaliyokuwwa yakijiri ukumbini humo.
Comments