Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf
Mzimba, mmoja wa wazee maarufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans
(YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita
Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni
na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais
Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. Picha na IKULU
Comments