Monday, March 18, 2013

TFF YAPOKEA BARUA TOKA UONGOZI HALALI WA SIMBA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.

Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.


Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.


Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo. HABARI NA FATHER KIDEVU http://mrokim.blogspot.com/2013/03/tff-yapokea-barua-toka-uongozi-halali-wa.html

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...