Wednesday, March 27, 2013

Rais Jakaya Kikwete Afunga Mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi yumo mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya jana katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo jana yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani jana
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

  Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha 835  Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde  Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata jana huko Ruvu
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT jana.Picha Zote za Tanga na Hussein Semdoe

No comments: