Monday, March 11, 2013

Ziara ya Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue Shirika la Nyumba la Taifa

Nyumba za mradi wa nyumba za gharama nafuu Kigamboni Housing Estate (Kibada) zilizotembelewa na  Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipofanya ziara ya siku nzima kupata taarifa na kukagua miradi mbalimbali. Shirika linajenga jumla ya nyumba 290 katika eneo hilo

 Baadhi ya nyumba za mradi wa nyumba za gharama nafuu Kigamboni Housing Estate (Kibada) zilizotembelewa na  Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipofanya ziara ya siku nzima kupata taarifa na kukagua miradi mbalimbali. Shirika linajenga jumla ya nyumba 290 katika eneo hilo.
 Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Issack Peter akimpa maelezo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Kigamboni Housing Estate (Kibada) Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipowasili katika Shirika hilo ambapo alifanya ziara ya siku nzima kupata taarifa na kukagua miradi mbalimbali.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akishuhudia mojawapo ya nyumba za gharama nafuu Kigamboni Housing Estate (Kibada) jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu na kushoto kwake  ni Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Issack Peter


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu  akimtambulisha Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akimpa maelezo ya ujenzi wa mradi wa NHC Housing uliopo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipowasili katika Shirika hilo ambapo alifanya ziara ya siku nzima kupata taarifa na kukagua miradi mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu  akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo.

No comments: