Monday, March 18, 2013

SHANGWE ZA MAFANIKIO YA Bia ya Serengeti Lager

Kampeni Kabambe ya kuitangaza Bia ya SerengetiLager inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama TUPOPAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO imelitikisa mitaa na vitongoji vya jiji la Dar es Salaam jana. Huku pakiwa naburudani ya muziki ambayo iliashiria Shangwe za mafanikio, Msafara wa magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya SBL pamoja na Lori kubwa aina ya Scania Semitrailer likiwa limepambwa vilivyo na kuleta mvuto wa ajabu kwa Watanzania lilikatika mitaa mbalimbali ya jiji.
Msafara huo wa kutoa Shukrani kwa Watanzania ndani ya jiji la Dar es Salaam ulianzia katika Kiwanda cha SBL Temeke kisha kwenda hadi Mwembeyanga hadi Saba saba.
Shangwe hizo ziliendelea hadi Taifa, Chang’ombe, Kamata, Msimbazi, kisha msafara huo ukaingia baranbara ya uhuru, ukapita Ilala ukaja tokea Buguruni, ukaingia Barabara ya Mandela hadi Ubungo kisha ukapita Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, ukaelekea Sinza ukatokea Bamaga ukafuata barabara ya Bagamoyo hadi Victoria ukaingia Mwananyamala na kumalizia viwanja vya Biafra Kinondoni.
Aidha shsngwe hizo zilikuwa zikiendelea katika maeneo kadhaa ya sehemu za starehe za Miti Mirefu, Kimara, Jambo park jet Lumo, Huduma Mbagala na Airtel Pub Banana.
Magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya Serengeti yaliongoza msafara huo.

Ni mwendo wa Shangwe tu ulikuwa ukiemdxelea kila kona Gari hilo lilipopita. Mbali na kampeni hii katika Mitaa ambayo imeanzia jijini Dar es Salaam na pia itasambaa mikoani pia Matangazo katikia vituo vya televisheni, Redio, Magazeti na Blogs yatakuwa yanatoka pamoja na mitaani.
 Magari mengine yalikuwa Nyuma na kupambwa na chapa mbalimbali za Bidhaa za kampuni ya SBL.
Tupo Pamoja katika Shangwe za Mafanikio…

No comments: