Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitazama baadhi ya malighafi,
alipotembelea kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO), alipotembelea
kiwanda hicho mjini Beijing, leo. Wapili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo
Xiong Weiping.
KATIBU
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri anayeshughulikia
mambo ya chama katika Chama Cha Kikomunisti cha China, Wang Jiarui,
alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing,
China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu
wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia
masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui,
alipokutana naye leo kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde
cha aina ya 'Ujamaa', Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO)
kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na
ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo
nchini China.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kweneye kitabu maalum cha
wageni, katika kampuni ya Aluminum ya China ((CHINALCO). Kushoto ni Rais
wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili kushoto ni Katibu wa Jumuia ya
Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman Dadi.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo
na uongozi wa CHINALCO, Kinana na ujumbe huo walipotembelea kampuni
hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing, China.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zwadi ya pambo la Kichina, na
Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing,
Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi
14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Picha na Bashir Nkoromo
Comments