Tunapenda kuutaarifu umma ya kuwa kuna genge la watu wanaotumia jina la
mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata katika mtandao wa kijamii wa
Facebook ili kuwarubuni wasichana. Kuna ukurasa ujulikanao kama Flaviana Matata’s hutumika
kama moja ya ukurasa wa Mwanamitindo huyu kitu ambacho si kweli. Watu
hawa huwarubuni wasichana na kuwaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi kwa
mgongo wa Mwanamitindo huyu. Genge hili la uhalifu hudai kuwa kuna
‘kaka’ yake Flaviana ambaye hukutana na wasichana hawa na baada ya
mazungumzo anawalaghai kwa njia mablimbali. Pia wahusika hawa hutoza
kiasi cha pesa hata kufikia shilingi laki mbili (200,000 )kama tozo kwa
huduma hii ya kuwatafutia kazi nje ya nchi.
Compass Communications kama kampuni inayosimamia shughuli za Flaviana
Matata inatoa tahadhari kwa umma kuwa Flaviana Matata hahusiki kwa njia
yoyote na ukurasa huu au watu hawa.
Pia tunawatahadharisha wananchi kuwa wawe waangalifu kwani Flaviana
Matata hayuko katika biashara ya kumtafutia mtu yoyote kazi ya Uanamitindo popote pale.
Ukurasa halisi ya Flaviana Matata kwenye mtandaomwa Facebook ni “Flaviana Lavvy Matata” .
Hivi sasa tunaendelea kushirikiana na vyombo husika kwa kutoa taarifa
kuhusu uhalifu huu na tunaomba ushirikiano wenu pia Wanajamii.
Imetolewa na
Compass Communications
Comments