Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa India Nchini wasaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia) kwa pamoja na
Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw wakisaini Mkataba wa
Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chuo cha Diplomasia (CFR) cha
Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya India (ICWA). Uwekaji saini huo
ulifanyika Wizarani jana tarehe 19 Machi, 2013.
Bw. Haule akibadilishana Mkataba na Balozi Shaw mara baada ya kusaini.
Katibu Mkuu, Bw. Haule pamoja na Balozi Shaw wakionesha Mkataba huo.
Katibu Mkuu Bw. Haule akizungumza na
Balozi Shaw mara baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini mkataba wa
Ushirikiano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya
Utamaduni ya India.
Mhe. Balozi Shaw akichangia hoja wakati wa mazungumzo na Bw. Haule huku wajumbe wengine wakisikiliza.
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia,
Balozi Mohammed Maundi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia
na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairukiwakishuhudia uwekaji saini wa mkataba
huo.
Wajumbe wengine waliohudhuria katika
tukio hilo la uwekaji saini wa mkataba. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka
Ubalozi wa India hapa nchini, Bw. Gobal Krisha na Bw. Ali Ubwa, Afisa
Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Sheria.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa
Comments